Total Pageviews
Saturday, 22 July 2017
DOWNLOAD NA SIKILIZA WIMBO UITWAO "TUTAPATAJE WOKOVU", WIMBO WA KWAYA NZURI KUTOKA KWAYA YA "MWISENGE ADVENTIST CHOIR"
UNAPENDA MUZIKI MTAMU?........... #Mwisenge_Adventist_Church_Choir wanakuletea wimbo uitwao #Tutapataje_Wokovu.........Ingia na download.
https://gospelmusikcloud.com/track/tutapataje-wokovu/
HISTORIA YA WIMBO-MSIFU MUNGU
#Historia_Ya_Wimbo_Msifu_Mungu*
#PRAISE_GOD_FROM_WHOM_ALL_BLESSING_FLOW_
ππΏ Ni wimbo ambao ulitungwa na kuandikwa na *Bishop Thomas Ken*
ππΏ Katika kitabu cha nyimbo za Kristo kiitwacho, *"The United Methodist Hymnal"*..........wimbo huu upo No. 95.......katika kitabu kidogo cha kiswahili *"Nyimbo Za Kristo"* wimbo huu upo No. 12.
ππΏ Huko Marekani, kuna tarehe maalumu kila mwaka wa tukio liitwalo , *"Thanks Giving"* ambapo nyimbo hutumika na kutoa sadaka maalumu kwa Mungu, wimbo huu pamoja na nyimbo nyingine kama hizi hutumika sana kwa ajili ya Kumsifu na kumshukuru Mungu............
ππΏ Kitaalamu nyimbo hizi za kumsifu Mungu huitwa , *"Doxology"*........ neno hilo limetolewa katika Lugha ya kigiriki likimaanisha *"Glory Saying-Kusema Utukufu"* ........Yaani *"Holy Trinity-Utatu Mtakatifu"*
ππΏ *Bishop, Thomas Ken*, alizaliwa mwaka *1637 na akafa mwaka 1711*
Maisha yake wanasema kuwa alilelewa kama Yatima lakini alitunzwa na dada yake aliyeitwa *Anna* pamoja na shemeji yake aliyeitwa *Izaak Walton*. Walimpeleka katika shule ya wavulana tupu katika chuo cha *Winchester* toka (1651- 1656).......... na baada ya masomo yake alijiunga chuo kikuu cha *Hart Hall, Oxford, Na New College, Oxford ( BA 1661, MA 1664).
ππΏ Baada ya hapo aliapishwa kuwa *kasisi wa Anglican mwaka 1662, akipagwa katika kuhudumu katika parish mbalimbali nchini uingereza...........Pia mwaka (1679-1680) alichaguliwa kuwa chaplain wa *Princess Mary wa Orange*........
na mwaka (1683-1684) ,alikuwa chaplain wa *Mfalme wa uingereza, _Mfalme Charles II_*........... Lakini pia mwaka (1685) alichaguliwa kuwa *Bishop* wa *Bath na Wells*
ππΏ Wakati wa utawala wa *Mfalme James II*, Alifungwa katika *mnara wa London-Tower of London* kwa kosa la kutokubaliana na maazimio ya mfalme, ila baadaye walimrudisha kazini. Lakini pia wakati wa kuapishwa kwa mfalme mwingine aliyeitwa *Mfalme William III* , Ken alikataa kuapa kumtii na kufanya naye kazi. Kwa hiyo *Thomas Ken* aliacha kazi yake na akaishi maisha yake yote yaliyobakia katika nyumba ya familia yake *Bwana, Weymouth* huko *Wilshire*.
ππΏ Tarehe mahususi ya lini wimbo huu ulitungwa haifahamiki ila mwaka 1674 ndio tarehe ambapo wimbo ulionekana na kuanza kuimbwa katika mikusanyiko ya Wakristo.
*_HISTORIA YA WIMBO NA MAANA YA WIMBO_*
ππΏ Kuna nyimbo mbili ambazo ni *Awake my soul and with the Sun* na mwingine *Glory to thee, my God , This Night*...........Hizi nyimbo mbili ziliekezea hali ya Asubuhi ,Jioni na Usiku wa manane............nyimbo hizo alizipata katika chemba yake aliyokuwa akilala katika *Chuo cha Winchester* ,na alikumbuka kuwa ni vizuri kuelezea uzuri na upendo wa Mungu asubuhi sana, na ukweli wake wakati wa Usiku.
So, wimbo huu wa *Msifu Mungu*, Ken aliutunga kuelezea mandhari ya fikra hizo hizo kusema utukufu wa Mungu ( *Doxology*)
ππΏ Wimbo huu umeimbwa sana kuliko nyimbo zote katika Ibada za Wakristo duniani.
ππΏ Tazama *Zaburi 96: 11-12* na *Zaburi 150:6*
Uone Doxology ya wimbo upoje.
♻♻♻♻♻♻♻♻
*MUNGU AKUBARIKI*
Imeletwa kwenu na mimi mfasili wako *Polite-Trio*
Tukutane Wakati Mwingineπ€
Subscribe to:
Posts (Atom)