Total Pageviews

Wednesday, 6 September 2017

HYMN HISTORY

#HISTORIA_YA_WIMBO_NO. 131. *#Baba Anilinda Trust In God*
🎻🎻🎻🎻🎻
katika video ,wanaitwa #Harmonizing_Fouth wakiuimba huu wimbo..........old school song.
Tumekuwa tukisikia nyimbo flani flani za zamani ambazo kwa namna ya pekee zinatukumbusha matendo makuu ambayo Mungu ametutendea.
👉 Huu wimbo ulitokea kuandikwa na William C. Martin ( *#1864-1914*), ambaye alikuwa Mchungaji wa kanisa. Vyanzo vinasema kuwa mtu wa kumpa hongera katika wimbo huu ni mtungaji mahiri duniani , *#Charles_Hutchinson_Gabriel* ( *#1856-1932* ) ,inawezekana ndiye aliyeandika wimbo huo ila sio mtoa maneno, *#Gabriel* ambaye inasemekana ametunga nyimbo *#7000* hadi *#8000* ambazo nyingi zinapatikana katika vitabu vya *#Nyimbo_za_Kristo.*
👉 Watungaji wengi wa nyimbo walikulia katika mashamba au huko vijijini na hata baba yake *#Charles_Gabriel* alikuwa akiongoza waimbaji katika shule ya huko kwao, na *#Charles_Gabriell* alikuwa akiupenda muziki. Inasemekana alijifunza pekee yake kupiga *#Organi_ya familia*. na hata hivyo alikuwa ana elimu flani kutoka shuleni iliyo msaidia. Alianzisha kikundi chake cha uimbaji na kukiongoza pekee yake na kuimba sehemu mbalimbali akiwa na miaka 17.
🎻🎸🎺🎷🥁🎹🎼🎤🎻
👉 Watu wanasema kuwa *#Mchungaji* wa kanisa la kwanza la *#Presbyterian* lililopo huko *#Wilton_Lowa*, alimwona *#Charless_Gabriel* akiwa katika matembezi yake huko mjini. Alimwita na kumuuliza ,kama anaweza akatengeneza wimbo mzuri utakao endana na hubiri lake. Yule mchungaji ambaye ni *#William_C_Martin* ,alimweleza hubiri lake lote *#Kijana_Gabriel* na baada ya week moja *#Gabriell* alikuwa kashauandika huo wimbo, kwani alitengeneza maneno na ala yake ( *#Instrument_music* ).
🎼🎼🎼🎼🎼🎼🎼
👉 Kwa hiyo haijalishi kuwa nani aliuandika wimbo huo lakini maneno hayo ni maalumu sana.............. [ Mara zote ni rahisi sana kumwamini Mungu na kumtumainia wakati mambo yako yanapo kuwa yamefanikiwa na huna tatizo lolote, ila matatizo yakianza, ni rahisi sana kuogopa na kusononeka kuwa kwa nini Mungu amekuacha....] ...........Ila wimbo huu unatukumbusha kuwa tunatakiwa kumwamini Mungu wakati wote, hata wakati wa dhoruba kali na vita vikali safarini au katika mabonde na majabari ya tabu. Yeye yuko pale kutulinda na kutuangazia wakati wa taabu hizo na changamoto mbalimbali za maisha.
🎤🎤🎤🎤🎤🎤🎤🎤
👉 Kubali wimbo huu ukukumbushe ni Mungu tu na ufalme wake ndio unaotakiwa uutumainie katika wakati mgumu na wakati wa raha maishani mwako.
👇🏼👇🏼👇🏼
🎧🎧🎧🎧🎧🎧🎧
(1) I trust in God wherever I may be,
Upon the land or on the rolling sea,
For, come what may, from day to day,
My heav'nly Father watches over me.
I trust in God, I know He cares for me,
On mountain bleak or on the stormy sea;
Tho' billows roll, He keeps my soul,
My heavn'ly Father watches over me.
🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳
Imetayarishwa na mimi *#Polite_Trio_Harrison*
Mbarikiwe.

No comments:

Post a Comment